الحجر
Al-Hijr
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlif Lam Ra. (A. L. R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWaache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Malaika wote pamoja walimsujudia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula
- Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka siku ya wakati maalumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIla waja wako walio safika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIna milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWaambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa uwape khabari za wageni wa Ibrahim.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIla mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakaja watu wa mji ule nao furahani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniUkelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ukelele ukawatwaa asubuhi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniUsivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKama hivyo tuliwateremshia walio gawa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wakaifanya Qur'ani vipande vipande.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa waliyo kuwa wakiyatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.