المؤمنون
Al-Mu'minun
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniHAKIKA wamefanikiwa Waumini,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao ni wanyenyekevu katika Sala zao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanatoa Zaka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanazilinda tupu zao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao Sala zao wanazihifadhi -
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio warithi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa juu yao na juu ya marikebu mnabebwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa zamani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakubwa katika watu wake walio kufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe katika maisha ya dunia, walisema: Huyu si chochote ila ni binaadamu kama nyinyi; anakula mlacho, na anakunywa mnywacho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHivyo anakuahidini ati ya kwamba mtakapo kufa na mkawa udongo na mifupa kuwa mtatolewa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHayawi! Hayawi hayo mnayo ahidiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi hatutafufuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa kumuamini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukaleta baada yao vizazi vingine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEnyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waache katika ghafla yao kwa muda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyo wapa mali na watoto
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMsiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Yeye ndiye aliye kuenezeni katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali wanasema kama walivyo sema watu wa kwanza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniTuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola wangu Mlezi! Usinijaalie katika watu madhaalimu hao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Sisi ni waweza wa kukuonyeshsa tuliyo waahidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAma wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMoto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmetukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.