مريم
Maryam
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniKaf Ha Ya A'yn S'ad
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimesha fikia ukongwe katika uzee?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akawatokea watu wake kutoka mihirabuni. Akawaashiria: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mchamungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari mua'si.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?
- Ali Muhsin Al-Barwani(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniPakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi?
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHaiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basi ole wao hao walio kufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayo tufikia! Lakini madhaalimu sasa wamo katika upotofu ulio dhaahiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa waonye siku ya majuto itapo katwa amri. Nao wamo katika ghafla, wala hawaamini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo mwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyo sikia, na visivyo ona, na visivyo kufaa chochote?
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe baba yangu! Kwa yakini imenifikia ilimu isiyo kufikia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza Njia Iliyo Sawa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe baba yangu! Usimuabudu Shet'ani. Hakika Shet'ani ni mwenye kumuasi Mwingi wa Rehema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe baba yangu! Hakika mimi naogopa isikupate adhabu inayo toka kwa Mwingi wa Rehema ukaja kuwa mwenziwe Shet'ani.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali kwa muda!
- Ali Muhsin Al-Barwani(Ibrahim) akasema: Salamun a'laika! Amani iwe juu yako! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNami najitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi alipo jitenga nao na yale waliyo kuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli Nabii.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimuinua daraja ya juu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa walio tubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wake katika siri. Hakika ahadi yake hapana shaka itafika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo hawatasikia upuuzi, ila Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamngu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Nao watasema:) Wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na udumu katika ibada yake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mwanaadamu husema: Hivyo, nitakapo kufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashet'ani; kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu, nao wamepiga magoti!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha kwa yakini tutawatoa katika kila kundi wale miongoni mwao walio zidi kumuasi Arrahmani, Mwingi wa Rahema..
- Ali Muhsin Al-BarwaniTena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanao stahiki kuunguzwa humo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tutawaokoa wale walio mchamngu; na tutawaacha madhaalimu humo wamepiga magoti.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, walio kufuru huwaambia walio amini: Lipi katika makundi mawili lenye cheo kizuri na lilio bora barazani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kaumu ngapi tuliziangamiza zilizo kuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi kwa kuwatazama!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingi wa Rahema atawapururia muda mpaka wayaone waliyo onywa - ama ni adhabu au ni Saa. Hapo ndipo watapo jua ni nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu. Na mema yenye kudumu ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe, umemwona aliye zikanya Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Tutaandika anayo yasema, tutamkunjulia muda wa adhabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tutamrithi hayo anayo yasema, na atatufikia mtupu peke yake!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wamechukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani huoni ya kwamba tumewatuma mashet'ani kwa makafiri wawachochee kwa uchochezi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahisabia idadi ya siku zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku tutayo wakusanya wachamngu kuwapeleka kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni wageni wake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawachunga wakhalifu kuwapeleka Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale walio chukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema..
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
- Ali Muhsin Al-BarwaniZinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniYeye hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wachamngu, na uwaonye kwayo watu wabishi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kaumu ngapi tumezihiliki kabla yao. Je! Unawaona hata mmoja katika wao au unasikia hata mchakato wao?