طه
Taha
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniT'AHA!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMateremsho yatokayo kwa aliye umba ardhi na mbingu zilizo juu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniArrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na viliomo baina yao, na viliomo chini ya ardhi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ukinyanyua sauti kwa kusema... basi hakika Yeye anajua siri na duni kuliko siri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa je! Imekufikia hadithi ya Musa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Saa itakuja bila ya shaka. Nimekaribia kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyo yafanya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hivyo asikukengeushe nayo yule ambaye haiamini na akafuata pumbao lake ukaja kuhiliki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Itupe, ewe Musa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa uambatishe mkono wako kwenye ubavu. Utatoka mweupe pasipo kuwa na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyengine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa unifanyie nyepesi kazi yangu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWapate kufahamu maneno yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nipe waziri katika watu wangu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHarun, ndugu yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwake yeye niongeze nguvu zangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa umshirikishe katika kazi yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli tukutakase sana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukukumbuke sana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Wewe unatuona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine...
- Ali Muhsin Al-BarwaniPale tulipo mfunulia mama yako yaliyo funuliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniYa kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo tokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniDada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Musa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anaye kadhibisha na akapuuza.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliye kipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Nini hali ya karne za kwanza?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ilimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za mimema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wenye akili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tunakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulimwonyesha ishara zetu zote. Lakini alikadhibisha na akakataa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ewe Musa! Hivyo umetujia kututoa katika nchi yetu kwa uchawi wako?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi sisi hakika tutakueletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali patapo kuwa sawa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu; na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Firauni akarudi na akatengeneza hila yake, kisha akaja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMusa akamwambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uwongo, asije akakufutilieni mbali kwa adhabu. Na mwenye kuzua lazima ashindwe!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakazozana kwa shauri yao wenyewe kwa wenyewe, na wakanong'ona kwa siri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wao, na waondoe mila zenu zilizo bora kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakaye shinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ewe Musa! Je! Utatupa wewe, au tutakuwa sisi wa kwanza kutupa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinapiga mbio.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Musa akaingia khofu nafsi yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukasema: Usikhofu! Hakika wewe ndiye utakaye shinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyo viunda. Hakika walivyo unda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wachawi wakaangushwa wanasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa!
- Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya maisha ya duniani tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi ulio tulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ataye mjia Mola wake Mlezi naye ni mkhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa atakaye mjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja wangu, na uwapigie njia kavu baharini. Usikhofu kukamatwa, wala usiogope.
- Ali Muhsin Al-BarwaniFirauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini kilicho wafudikiza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Firauni aliwapoteza watu wake wala hakuwaongoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEnyi Wana wa Israili! Hakika tulikuokoeni na adui yenu, na tukakuahidini upande wa kulia wa mlima. Na tulikuteremshieni Manna na Salwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni, wala msiruke mipaka katika hayo, isije ikakushukieni ghadhabu yangu. Na inaye mshukia ghadhabu yangu basi huyo ameangamia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anaye tubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kilicho kutia haraka ukawaacha watu wako, ewe Musa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuatia. Na nimefanya haraka kukujia, Mola wangu Mlezi, ili uridhike.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMusa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi yangu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa khiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri Msamaria.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala hakuweza kuwadhuru wala kuwafaa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na t'iini amri yangu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hatutaacha kumuabudu mpaka Musa atapo rejea kwetu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho kuzuia, ulipo waona wamepotea,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHata usinifuate? Je, umeasi amri yangu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Niliona wasiyo yaona wao, nikashika gao katika unyao wa Mtume. Kisha nikalitupa. Na hivi ndivyo ilivyo nielekeza nafsi yangu.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya baharini atawanyike.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mungu wenu ni Allah, Mwenyezi Mungu, tu. Hapana Mungu isipo kuwa Yeye. Ujuzi wake umeenea kila kitu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNamna hivi tunakuhadithia katika khabari za yaliyo tangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtakaye jitenga nayo, basi kwa yakini Siku ya Kiyama atabeba mzigo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWadumu humo. Na ni mzigo muovu kwao kuubeba Siku ya Kiyama!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku litakapo pulizwa barugumu, na tukawakusanya wakhalifu Siku hiyo, hali macho yao ya kibuluu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatanong'onezana wao kwa wao: Hamkukaa ila siku kumi tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tunajua zaidi watakayo yasema, atakapo sema mbora wao katika mwendo: Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanakuuliza khabari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ataiacha tambarare, uwanda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHutaona humo mdidimio wala muinuko.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo watamfuata muitaji asiye na upotofu. Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani Mwingi wa Rahema. Basi husikii ila mchakato na mnong'ono.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo uombezi haufai kitu, ila wa aliye mruhusu Arrahmani Mwingi wa Rehema na akamridhia kusema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniYeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye vilivyo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhulma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa anaye tenda mema, naye ni Muumini, basi hatakhofu kudhulumiwa wala kupunjwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa namna hivi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo maonyo ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmetukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakasujudu, isipo kuwa Iblisi, alikataa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wa mkeo. Basi asikutoeni katika Bustani hii, mkaingia mashakani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini Shet'ani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi milele na ufalme usio koma?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustani. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha Mola wake Mlezi akamteuwa, naye akamkubalia toba yake, naye akamwongoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hivi ndivyo tutakavyo mlipa kila apitaye kiasi, na asiye amini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Haikuwabainikia tu; vizazi vingapi tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye akili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi na muda ulio wekwa, bila ya shaka inge fika adhabu (hapa hapa).
- Ali Muhsin Al-BarwaniYavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla halijachwa, na nyakati za usiku pia umtakase, na ncha za mchana ili upate ya kukuridhisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala usivikodolee macho tulivyo wastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na inadumu zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa mchamngu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walisema: Kwa nini hakutuletea muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Je! Haikuwafikilia dalili wazi ya yaliyomo katika Vitabu vya kale?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa tuliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangeli sema: Ewe Mola wetu Mlezi! Kwa nini usituletee Mtume tukazifuata ishara zako kabla hatujadhilika na kuhizika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni! Hivi karibuni mtajua nani mwenye njia sawa na nani aliye ongoka.