الشعراء

Ash-Shu'ara

Sura ya 26 · ya Makka · aya 227 · Mpangilio wa kuteremshwa: 47

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniT'aa Siin Miim. (T'. S. M.)
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatu wa Firauni. Hawaogopi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaachilie Wana wa Israili wende nasi.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniFirauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAnataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMusa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMusa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHapo wachawi walipinduka wakasujudu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa Musa na Harun.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNao wanatuudhi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukawatoa katika mabustani na chemchem,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa makhazina, na vyeo vya hishima,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakawafuata lilipo chomoza jua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawajongeza hapo wale wengine.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawazamisha hao wengine.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wasomee khabari za Ibrahim.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu yanakufaeni, au yanakudhuruni?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mmewaona hawa mnao waabudu-
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNyinyi na baba zenu wa zamani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa unijaalie katika warithi wa Bustani za neema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala usinihizi Siku watapo fufuliwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Pepo itasogezwa kwa wachamngu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBadala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa majeshi ya Ibilisi yote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hawakutupoteza ila wale wakosefu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hatuna waombezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala rafiki wa dhati.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLaiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKina A'd waliwakanusha Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmekupeni wanyama wa kufuga na wana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mabustani na chemchem.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHaya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala sisi hatutaadhibiwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKina Thamud waliwakanusha Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKatika mabustani, na chemchem?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatu wa Lut'i waliwakanusha Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawaangamiza wale wengine.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatu wa Machakani waliwakanusha Mitume.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniShuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTimizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa pimeni kwa haki iliyo nyooka;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmeuteremsha Roho muaminifu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJuu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNamna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHawataiamini mpaka waione adhabu chungu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa watasema: Je, tutapewa muhula?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji -
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hao wametengwa na kusikia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye anakuona unapo simama,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mageuko yako kati ya wanao sujudu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba wao husema wasiyo yatenda?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.