ص

Sad

Sura ya 38 · ya Makka · aya 88 · Mpangilio wa kuteremshwa: 38

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniS'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAti yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWalikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSubiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWalipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniEwe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wengine wafungwao kwa minyororo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu.
  1. Ali Muhsin Al-Barwani(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHumo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHaya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNdio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNdio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa adhabu nyenginezo za namna hii.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Hii ni khabari kubwa kabisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbayo nyinyi mnaipuuza.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHaikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Malaika wakat'ii wote pamoja.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka siku ya wakati maalumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Haki! Na haki ninaisema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSema (Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.