الصافات
As-Saffat
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa wanao jipanga kwa safu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa wenye kukataza mabaya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa wenye kusoma Ukumbusho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kulinda na kila shet'ani a'si.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo kumbushwa hawakumbuki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHata baba zetu wa zamani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu -
- Ali Muhsin Al-BarwaniBadala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
- Ali Muhsin Al-BarwaniMna nini? Mbona hamsaidiani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali hii leo, watasalimu amri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatakabiliana wao kwa wao kuulizana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio watakao pata riziki maalumu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMatunda, nao watahishimiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Bustani za neema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWako juu ya viti wamekabiliana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
- Ali Muhsin Al-BarwaniKinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakina madhara, wala hakiwaleweshi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWaingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki
- Ali Muhsin Al-BarwaniAliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema: Je! Nyie mnawaona?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Sisi hatutakufa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa mfano wa haya nawatende watendao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika waliwakuta baba zao wamepotea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawazamisha wale wengine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akapiga jicho kutazama nyota.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao wakamwacha, wakampa kisogo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMna nini hata hamsemi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakamjia upesi upesi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukambashiria mwana aliye mpole.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTulimwita: Ewe Ibrahim!
- Ali Muhsin Al-BarwaniUmekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe salama kwa Ibrahim!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe salama kwa Musa na Haruni!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo waambia watu wake: Hamwogopi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe salama kwa Ilyas.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawaangamiza wale wengineo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSamaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHamkumbuki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu mnayo hoja iliyo wazi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSubhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hakika nyinyi na mnao waabudu
- Ali Muhsin Al-BarwaniHamwezi kuwapoteza
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walikuwapo walio kuwa wakisema:
- Ali Muhsin Al-BarwaniTungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini waliukataa. Basi watakuja jua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniYa kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waachilie mbali kwa muda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa watazame, nao wataona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Wanaihimiza adhabu yetu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa waache kwa muda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tazama, na wao wataona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSubhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Salamu juu ya Mitume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.