الزخرف
Az-Zukhruf
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniH'a Mim
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa Kitabu kinacho bainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye hikima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyo kufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jike na dume, na akakufanyieni marikebu na wanyama mnao wapanda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeli weza kufanya haya wenyewe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhaahiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana...?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye bainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walisema: Kwa nini Qur'ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazo pandia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliye mneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala asikuzuilieni Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnit'ii mimi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEnyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIngieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMnayo humo matunda mengi mtakayo yala.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmetakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A'rshi, na hayo wanayo msifia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua.