الدخان
Ad-Dukhan
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniH'a Mim
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa Kitabu kinacho bainisha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima,
- Ali Muhsin Al-BarwaniJambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wao wanacheza katika shaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,
- Ali Muhsin Al-BarwaniUtakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mimea na vyeo vitukufu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa neema walizo kuwa wakijistareheshea!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniYa Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hawa wanasema:
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mti wa Zaqqum,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi chakula cha mwenye dhambi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
- Ali Muhsin Al-BarwaniKama kutokota kwa maji ya moto.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOnja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika mabustani na chemchem,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNgoja tu, na wao wangoje pia.