ق
Qaf
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniQaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.
- Ali Muhsin Al-BarwaniYawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHaya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea-
- Ali Muhsin Al-Barwani(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo.