الذاريات
Adh-Dhariyat
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa pepo zinazo tawanya,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo beba mizigo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo kwenda kwa wepesi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo gawanya kwa amri,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mbingu zenye njia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWazushi wameangamizwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wameghafilika katika ujinga.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOnjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalikuwa wakilala kidogo tu usiku.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniTuwatupie mawe ya udongo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniYaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHaukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.