الواقعة
Al-Waqi'ah
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniLitakapo tukia hilo Tukio
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana cha kukanusha kutukia kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLiteremshalo linyanyualo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniItakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima itapo sagwasagwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe mavumbi yanayo peperushwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyinyi mtakuwa namna tatu:-
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wa mbele watakuwa mbele.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio watakao karibishwa
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Bustani zenye neema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniFungu kubwa katika wa mwanzo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wachache katika wa mwisho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakiviegemea wakielekeana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa matunda wayapendayo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyama za ndege kama wanavyo tamani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mahurulaini,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika mikunazi isiyo na miba,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa migomba iliyo pangiliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kivuli kilicho tanda,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa maji yanayo miminika,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa matunda mengi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHayatindikii wala hayakatazwi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa matandiko yaliyo nyanyuliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tutawafanya vijana,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanapendana na waume zao, hirimu moja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa ajili ya watu wa kuliani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniFungu kubwa katika wa mwanzo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa fungu kubwa katika wa mwisho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kivuli cha moshi mweusi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSi cha kuburudisha wala kustarehesha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu baba zetu wa zamani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Hakika wa zamani na wa mwisho
- Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mti huo mtajaza matumbo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnaona makulima mnayo yapanda?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniTungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMkisema: Hakika sisi tumegharimika;
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali sisi tumenyimwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnayaona maji mnayo yanywa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniTungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnauona moto mnao uwasha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi naapa kwa maanguko ya nyota,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Kitabu kilicho hifadhiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana akigusaye ila walio takaswa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniYawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyinyi wakati huo mnatazama!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akiwa katika watu wa upande wa kulia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi karamu yake ni maji yanayo chemka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kutiwa Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hii ndiyo haki yenye yakini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.