الرحمن
Ar-Rahman
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniArrah'man, Mwingi wa Rehema
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmefundisha Qur'ani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmemuumba mwanaadamu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkamfundisha kubaini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJua na mwezi huenda kwa hisabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli msidhulumu katika mizani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nafaka zenye makapi, na rehani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnaziendesha bahari mbili zikutane;
- Ali Muhsin Al-BarwaniBaina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKila kilioko juu yake kitatoweka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniVinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniTutakuhisabuni enyi makundi mawili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniEnyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniItakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBustani zenye matawi yaliyo tanda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo katika kila matunda zimo namna mbili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKama kwamba wao ni yakuti na marijani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniZa kijani kibivu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa chemchem mbili zinazo furika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniImo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo wamo wanawake wema wazuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHajawagusa mtu wala jini kabla yao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniLimetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.