القلم

Al-Qalam

Sura ya 68 · ya Makka · aya 52 · Mpangilio wa kuteremshwa: 2

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika wewe una tabia tukufu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKaribu utaona, na wao wataona,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi usiwat'ii wanao kadhibisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMtapitapi, apitaye akifitini,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAti kwa kuwa ana mali na watoto!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAnapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTutamtia kovu juu ya pua yake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala hawakusema: Mungu akipenda!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLikawa kama usiku wa giza.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAsubuhi wakaitana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYa kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi walikwenda na huku wakinong'onezana,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYa kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBali tumenyimwa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAsaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNamna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMna nini? Mnahukumu vipi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKuwa mtapata humo mnayo yapenda?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMacho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima -
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu iko kwao siri, basi wao wanaiandika?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.