الحاقة
Al-Haqqah
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukio la haki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNini hilo Tukio la haki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniThamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMaji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo ndio Tukio litatukia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Bustani ya juu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMatunda yake yakaribu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWaambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala nisingeli jua nini hisabu yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLaiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMali yangu hayakunifaa kitu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMadaraka yangu yamenipotea.
- Ali Muhsin Al-Barwani(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha mtupeni Motoni!
- Ali Muhsin Al-BarwaniTena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hahimizi kulisha masikini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniChakula hicho hawakili ila wakosefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi naapa kwa mnavyo viona,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa msivyo viona,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.