العاديات

Al-'Adiyat

Sura ya 100 · ya Makka · aya 11 · Mpangilio wa kuteremshwa: 14

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakishambulia wakati wa asubuhi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuku wakitimua vumbi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakijitoma kati ya kundi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa yakakusanywa yaliomo vifuani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!