القارعة

Al-Qari'ah

Sura ya 101 · ya Makka · aya 11 · Mpangilio wa kuteremshwa: 30

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniInayo gonga!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNini Inayo gonga?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHuyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi Moto mkali!