الزلزلة

Az-Zalzalah

Sura ya 99 · ya Madina · aya 8 · Mpangilio wa kuteremshwa: 93

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniItakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa itakapo toa ardhi mizigo yake!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mtu akasema: Ina nini?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo itahadithia khabari zake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa anaye tenda chembe ya uovu atauona!