التكاثر

At-Takathur

Sura ya 102 · ya Makka · aya 8 · Mpangilio wa kuteremshwa: 16

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKumekushughulisheni kutafuta wingi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka mje makaburini!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Mtakuja jua!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.