الهمزة

Al-Humazah

Sura ya 104 · ya Makka · aya 9 · Mpangilio wa kuteremshwa: 32

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniOle wake kila safihi, msengenyaji!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAliye kusanya mali na kuyahisabu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAnadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nani atakujuvya ni nini H'ut'ama?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMoto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao unapanda nyoyoni.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika huo utafungiwa nao
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwenye nguzo zilio nyooshwa.