الطور
At-Tur
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mlima wa T'ur,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Kitabu kilicho andikwa
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika ngozi iliyo kunjuliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa Nyumba iliyo jengwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa dari iliyo nyanyuliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa bahari iliyo jazwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana wa kuizuia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanacheza katika mambo ya upuuzi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu,
- Ali Muhsin Al-Barwani(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniUingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWatapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWataelekeana wakiulizana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWaseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa;
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.