النجم
An-Najm
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa nyota inapo tua,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hatamki kwa matamanio.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmemfundisha aliye mwingi wa nguvu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenye kutua, akatulia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaye yuko juu kabisa upeo wa macho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akakaribia na akateremka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAkamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMoyo haukusema uwongo uliyo yaona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akamwona mara nyingine,
- Ali Muhsin Al-BarwaniPenye Mkunazi wa mwisho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKaribu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mmemuona Lata na Uzza?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Manaat, mwingine wa tatu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuo ni mgawanyo wa dhulma!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti mtu anakipata kila anacho kitamani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Umemwona yule aliye geuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akatoa kidogo, kisha akajizuia?
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniYa kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba vitendo vyake vitaonekana?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
- Ali Muhsin Al-BarwaniKutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Thamudi hakuwabakisha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniVikaifunika vilivyo funika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKiyama kimekaribia!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Mnayastaajabia maneno haya?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnacheka, wala hamlii?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNanyi mmeghafilika?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.