القمر
Al-Qamar
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniSaa imekaribia, na mwezi umepasuka!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha;
- Ali Muhsin Al-BarwaniMacho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIkawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniUkiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniThamudi waliwakanusha Waonyaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi onjeni adhabu na maonyo yangu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKatika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.