المعارج
Al-Ma'arij
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniMuulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia -
- Ali Muhsin Al-BarwaniKutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMalaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi subiri kwa subira njema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wao wanaiona iko mbali,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Sisi tunaiona iko karibu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima itakuwa kama sufi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIjapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mkewe, na nduguye,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa jamaa zake walio kuwa wakimkimu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniUnao babua ngozi ya kichwa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniUtamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mtu ameumbwa na papara.
- Ali Muhsin Al-BarwaniInapo mgusa shari hupapatika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa inapo mgusa kheri huizuilia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa wanao sali,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanadumisha Sala zao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao katika mali yao iko haki maalumu
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanahifadhi tupu zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi -
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambao wanazihifadhi Sala zao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio watakao hishimiwa Peponi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMakundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMacho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa.