نوح

Nuh

Sura ya 71 · ya Makka · aya 28 · Mpangilio wa kuteremshwa: 71

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYa kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAtakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena niliwaita kwa uwazi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAtakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIli mtembee humo katika njia zilizo pana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakapanga vitimbi vikubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.