الجن
Al-Jinn
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniInaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIla nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniYeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.