المزمل
Al-Muzzammil
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe uliye jifunika!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKesha usiku kucha, ila kidogo tu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNusu yake, au ipunguze kidogo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hakika mchana una shughuli nyingi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.