المدثر

Al-Muddaththir

Sura ya 74 · ya Makka · aya 56 · Mpangilio wa kuteremshwa: 4

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniEwe uliye jigubika!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSimama uonye!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mola wako Mlezi mtukuze!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nguo zako, zisafishe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa yaliyo machafu yahame!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi litapo pulizwa barugumu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa makafiri haitakuwa nyepesi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNiache peke yangu na niliye muumba;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nikamjaalia awe na mali mengi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wana wanao onekana,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha anatumai nimzidishie!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hakika yeye alifikiri na akapima.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ameangamia! Vipi alivyo pima!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena ameangamia! Vipi alivyo pima!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akatazama,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akakunja kipaji, na akanuna.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHaya si chochote ila kauli ya binaadamu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHaubakishi wala hausazi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUnababua ngozi iwe nyeusi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJuu yake wapo kumi na tisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Naapa kwa mwezi!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku unapo kucha!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa asubuhi inapo pambazuka!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi onyo kwa binaadamu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa watu wa kuliani.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKhabari za wakosefu:
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi nini kilicho kupelekeni Motoni?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala hatukuwa tukiwalisha masikini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka yakini ilipo tufikia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanao mkimbia simba!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAti kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi anaye taka atakumbuka.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.