القيامة
Al-Qiyamah
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNinaapa kwa Siku ya Kiyama!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi jicho litapo dawaa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mwezi utapo patwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa likakusanywa jua na mwezi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa! Hapana pa kukimbilia!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ingawa atatoa chungu ya udhuru.
- Ali Muhsin Al-BarwaniUsiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha ni juu yetu kuubainisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnaacha maisha ya Akhera.
- Ali Muhsin Al-BarwaniZipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
- Ali Muhsin Al-BarwaniZinamwangallia Mola wao Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniZitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa pakasemwa: Nani wa kumganga?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali alikanusha, na akageuka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wako, ole wako!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha Ole wako, ole wako!
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?