الانسان
Al-Insan
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNi chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,
- Ali Muhsin Al-BarwaniVya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJuu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHumuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.