المرسلات
Al-Mursalat
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo vuma kwa kasi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zikaeneza maeneo yote!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo farikisha zikatawanya!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa zinazo peleka mawaidha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa kuudhuru au kuonya,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakati nyota zitakapo futwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu zitakapo pasuliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima itakapo peperushwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mitume watakapo wekewa wakati wao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa siku ya kupambanua!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukawafuatilizia walio fuatia?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
- Ali Muhsin Al-BarwaniMpaka muda maalumu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniTukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
- Ali Muhsin Al-BarwaniWalio hai na maiti?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao walio kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniIkiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao walio kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa matunda wanayo yapenda,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
- Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo hao wanao kanusha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi maneno gani baada ya haya watayaamini?