النبإ
An-Naba
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniWANAULIZANA nini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniIle khabari kuu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbayo kwayo wanakhitalifiana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLa! Karibu watakuja jua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTena la! Karibu watakuja jua.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima kama vigingi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukakuumbeni kwa jozi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukaufanya usiku ni nguo?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIli tutoe kwayo nafaka na mimea,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mabustani yenye miti iliyo kamatana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu zitafunguliwa, ziwe milango,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Jahannamu inangojea!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa walio asi ndio makaazi yao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakae humo karne baada ya karne,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
- Ali Muhsin Al-BarwaniIla maji yamoto sana na usaha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNdio jaza muwafaka.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wachamngu wanastahiki kufuzu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMabustani na mizabibu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wake walio lingana nao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bilauri zilizo jaa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHawatasikia humo upuuzi wala uwongo -
- Ali Muhsin Al-BarwaniMalipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniMola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSiku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!