النازعات

An-Nazi'at

Sura ya 79 · ya Makka · aya 46 · Mpangilio wa kuteremshwa: 81

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa wanao toa kwa upole,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanao ogelea,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakishindana mbio,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakidabiri mambo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKifuate cha kufuatia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo nyoyo zitapiga piga,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMacho yatainama chini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Imekufikia hadithi ya Musa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUmwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi alimwonyesha Ishara kubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini aliikadhibisha na akaasi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkakusanya watu akanadi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima akaisimamisha,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa nafuu yenu na mifugo yenu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ama yule aliye zidi ujeuri,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akakhiari maisha ya dunia,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUna nini wewe hata uitaje?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.