عبس

'Abasa

Sura ya 80 · ya Makka · aya 42 · Mpangilio wa kuteremshwa: 24

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAlikunja kipaji na akageuka,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa sababu alimjia kipofu!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu atawaidhika, na mawaidha yamfae?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAma ajionaye hana haja,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWewe ndio unamshughulikia?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa si juu yako kama hakutakasika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAma anaye kujia kwa juhudi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaye anaogopa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNdio wewe unampuuza?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi anaye penda akumbuke.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZilizo inuliwa, zilizo takaswa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZimo mikononi mwa Malaika waandishi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatukufu, wema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmeangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa kitu gani amemuumba?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akamsahilishia njia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akamfisha, akamtia kaburini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha apendapo atamfufua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLa! Hajamaliza aliyo muamuru.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHebu mtu na atazame chakula chake.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukaotesha humo nafaka,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa zabibu, na mimea ya majani,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mizaituni, na mitende,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa matunda, na malisho ya wanyama;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa manufaa yenu na mifugo yenu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi utakapo kuja ukelele,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mamaye na babaye,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mkewe na wanawe -
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZitacheka, zitachangamka;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniGiza totoro litazifunika,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio makafiri watenda maovu.