التكوير
At-Takwir
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniJua litakapo kunjwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyota zikazimwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima ikaondolewa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanyama wa mwituni wakakusanywa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa bahari zikawaka moto,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nafsi zikaunganishwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa kosa gani aliuliwa?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa madaftari yatakapo enezwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu itapo tanduliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Jahannamu itapo chochewa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Pepo ikasogezwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
- Ali Muhsin Al-BarwaniZinazo kwenda, kisha zikajificha,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku unapo pungua,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa asubuhi inapo pambazuka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniMwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnaye t'iiwa, tena muaminifu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wala huyu mwenzenu hana wazimu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hii si kauli ya Shetani maluuni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi mnakwenda wapi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniHaikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.