الإنفطار

Al-Infitar

Sura ya 82 · ya Makka · aya 19 · Mpangilio wa kuteremshwa: 82

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMbingu itapo chanika,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nyota zitapo tawanyika,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bahari zitakapo pasuliwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa makaburi yatapo fukuliwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniEwe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKatika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWaandishi wenye hishima,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanayajua mnayo yatenda.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWataingia humo Siku ya Malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hawatoacha kuwamo humo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.