المطففين

Al-Mutaffifin

Sura ya 83 · ya Makka · aya 36 · Mpangilio wa kuteremshwa: 86

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao hao wapunjao!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Siku iliyo kuu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUnajua nini Sijjin?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKitabu kilicho andikwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniOle wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAnapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha wataingia Motoni!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKitabu kilicho andikwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWanakishuhudia walio karibishwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUtatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWatanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMuhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mchanganyiko wake ni Tasniim,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniChemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?