الإنشقاق
Al-Inshiqaq
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniItapo chanika mbingu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi itakapo tanuliwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAma atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa arudi kwa ahali zake na furaha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi huyo ataomba kuteketea.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ataingia Motoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHuyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku na unavyo vikusanya,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mwezi unapo pevuka,
- Ali Muhsin Al-BarwaniLazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wana nini hawaamini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBali walio kufuru wanakanusha tu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wabashirie adhabu chungu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniIsipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.