البروج

Al-Buruj

Sura ya 85 · ya Makka · aya 22 · Mpangilio wa kuteremshwa: 27

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mbingu yenye Buruji!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa siku iliyo ahidiwa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWameangamizwa watu wa makhandaki
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYenye moto wenye kuni nyingi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWalipo kuwa wamekaa hapo,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAtendaye ayatakayo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Zimekuwasilia khabari za majeshi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYa Firauni na Thamudi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBali hii ni Qur'ani tukufu
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Ubao Ulio Hifadhiwa.