الطارق

At-Tariq

Sura ya 86 · ya Makka · aya 17 · Mpangilio wa kuteremshwa: 36

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNi Nyota yenye mwanga mkali.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHapana nafsi ila inayo mwangalizi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmeumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniYatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku zitakapo dhihirishwa siri.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mbingu yenye marejeo!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa ardhi inayo pasuka!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika hii ni kauli ya kupambanua.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWala si mzaha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika wao wanapanga mpango.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mimi napanga mpango.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.