الأعلى

Al-A'la

Sura ya 87 · ya Makka · aya 19 · Mpangilio wa kuteremshwa: 8

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLitakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAliye umba, na akaweka sawa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ambaye amekadiria na akaongoa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa aliye otesha malisho,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akayafanya makavu, meusi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTutakusomesha wala hutasahau,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIla akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa tutakusahilishia yawe mepesi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAtakumbuka mwenye kuogopa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa atajitenga mbali nayo mpotovu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye atauingia Moto mkubwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTena humo hatakufa wala hawi hai.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniVitabu vya Ibrahimu na Musa.