الغاشية

Al-Ghashiyah

Sura ya 88 · ya Makka · aya 26 · Mpangilio wa kuteremshwa: 68

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo nyuso zitainama,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZikifanya kazi, nazo taabani.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZiingie katika Moto unao waka -
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSiku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniZitakuwa radhi kwa juhudi yao,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKatika Bustani ya juu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHawatasikia humo upuuzi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHumo imo chemchem inayo miminika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHumo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bilauri zilizo pangwa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa matakia safu safu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mazulia yaliyo tandikwa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa milima jinsi ilivyo thibitishwa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniWewe si mwenye kuwatawalia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini anaye rudi nyuma na kukataa,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!