الفجر
Al-Fajr
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa alfajiri,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa masiku kumi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa viwili viwili na kimoja kimoja,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku unapo pita,
- Ali Muhsin Al-BarwaniJe! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWa Iram, wenye majumba marefu?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Firauni mwenye vigingi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAmbao walifanya jeuri katika nchi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniWakakithirisha humo ufisadi?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAma mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
- Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hamhimizani kulisha masikini;
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniSivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAtasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniEwe nafsi iliyo tua!
- Ali Muhsin Al-BarwaniRejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ingia miongoni mwa waja wangu,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ingia katika Pepo yangu.