البلد
Al-Balad
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa Mji huu!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNawe unaukaa Mji huu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa naapa kwa mzazi na alicho kizaa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika tumemuumba mtu katika taabu.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti anadhani hapana yeyote ataye muweza?
- Ali Muhsin Al-BarwaniAnasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
- Ali Muhsin Al-BarwaniAti anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hatukumpa macho mawili?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ulimi, na midomo miwili?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukambainishia zote njia mbili?
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
- Ali Muhsin Al-BarwaniKumkomboa mtumwa;
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu kumlisha siku ya njaa
- Ali Muhsin Al-BarwaniYatima aliye jamaa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAu masikini aliye vumbini.
- Ali Muhsin Al-BarwaniTena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
- Ali Muhsin Al-BarwaniHao ndio watu wa kheri wa kuliani.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
- Ali Muhsin Al-BarwaniJuu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.