الشمس
Ash-Shams
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa jua na mwangaza wake!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mwezi unapo lifuatia!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mchana unapo lidhihirisha!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku unapo lifunika!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
- Ali Muhsin Al-BarwaniKisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika amefanikiwa aliye itakasa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika amekhasiri aliye iviza.
- Ali Muhsin Al-BarwaniKina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
- Ali Muhsin Al-BarwaniAlipo simama mwovu wao mkubwa,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
- Ali Muhsin Al-BarwaniLakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
- Ali Muhsin Al-BarwaniWala Yeye haogopi matokeo yake.