الليل

Al-Layl

Sura ya 92 · ya Makka · aya 21 · Mpangilio wa kuteremshwa: 9

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa usiku unapo funika!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mchana unapo dhihiri!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa Aliye umba dume na jike!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAma mwenye kutoa na akamchamngu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akaliwafiki lilio jema,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTutamsahilishia yawe mepesi.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akakanusha lilio jema,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniTutamsahilishia yawe mazito!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi nakuonyeni na Moto unao waka!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHatauingia ila mwovu kabisa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAnaye kadhibisha na kupa mgongo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa mchamngu ataepushwa nao,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniIla ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaye atakuja ridhika!