الضحى

Ad-Duhaa

Sura ya 93 · ya Makka · aya 11 · Mpangilio wa kuteremshwa: 11

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa mchana!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa usiku unapo tanda!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa akakukuta umepotea akakuongoa?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkakukuta mhitaji akakutosheleza?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi yatima usimwonee!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa anaye omba au kuuliza usimkaripie!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa neema za Mola wako Mlezi zisimlie.