الشرح
Ash-Sharh
Hati
Tafsiri
Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
- Ali Muhsin Al-BarwaniHatukukunjulia kifua chako?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukakuondolea mzigo wako,
- Ali Muhsin Al-BarwaniUlio vunja mgongo wako?
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa tukakunyanyulia utajo wako?
- Ali Muhsin Al-BarwaniBasi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
- Ali Muhsin Al-BarwaniHakika pamoja na uzito upo wepesi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa ukipata faragha, fanya juhudi.
- Ali Muhsin Al-BarwaniNa Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.