التين

At-Tin

Sura ya 95 · ya Makka · aya 8 · Mpangilio wa kuteremshwa: 28

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNaapa kwa tini na zaituni!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa Mlima wa Sinai!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNa kwa mji huu wenye amani!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniLakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?