العلق

Al-'Alaq

Sura ya 96 · ya Makka · aya 19 · Mpangilio wa kuteremshwa: 1

Hati
Tafsiri

Gusa neno la Kiarabu ili kuona usomaji, muundo na mzizi wake.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSoma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmemuumba binaadamu kwa tone la damu,
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniSoma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAmbaye amefundisha kwa kalamu.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAkijiona katajirika.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUmemwona yule anaye mkataza
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniMja anapo sali?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUmeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniAu anaamrisha uchamngu?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniUmeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniKwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniShungi la uwongo, lenye makosa!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniBasi na awaite wenzake!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniNasi tutawaita Mazabania!
  1. Ali Muhsin Al-BarwaniHasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!